Hayo yameripotiwa na televisheni ya Russia al Yaum ambayo imesema kuwa, kiwango cha mfumuko wa bei nchini Ujerumani katika mwezi Aprili 2022 imevunja rekodi ya tangu mwaka 1981 hasa katika bidhaa za petrokemikali.
Televisheni hiyo imenukuu ripoti ya Idara ya Takwimu ya Shirikisho la Ujerumani ikisema kuwa, bei za bidhaa kwa watumiaji zilipanda kwa asilimia 7.8 ikiliganishwa na muda kama huo mwaka uliopita na kwamba kiwango hicho hakijawahi kushuhudiwa kwa miongo kadhaa huko Ujerumani.
Hata hivyo Umoja wa Ulaya unajaribu kufifiliza jambo hilo kwa kudai katika ripoti yake kwamba ukuaji wa uchumi kwenye Ukanda wa Euro umepungua kwa asilimia 0.2 katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
Madai hayo yanakinzana kikamilifu na ripoti ya Idara ya Takwimu ya Shirikisho la Ujerumani ambayo imesema, mfumuko wa bei katika mwezi wa Aprili umevunja rekodi ya miaka 40 nchini humo.
Pamoja na kujaribu kufifiliza habari hiyo lakini Kituo cha Takwimu cha Umoja wa Ulaya (Eurostat), kimelazimika kusema kuwa, kiwango cha mfumuko wa bei katika nchi 19 wanachama wa Umoja wa Ulaya kilifikia asilimia 7.5, kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa kwenye ukanda huo tangu Umoja wa Ulaya ulipoanza kutoa takwimu zake mwaka 1997.
Ikumbukwe pia kuwa, tangu mwezi Novemba 2021 hadi hivi sasa, rekodi za mfumuko wa bei zinavunjwa kila mwezi katika nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.
342/